Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika imara baina ya UM na nchi wanachama ni muhimu kukomesha ukatili wa kingono:

Ushirika imara baina ya UM na nchi wanachama ni muhimu kukomesha ukatili wa kingono:

[caption id="attachment_323268" align="aligncenter" width="625"]taarifaatulkhare

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo alhamisi amesisitiza umuhimu wa ushirika imara baina ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama katika kusonga mbele na juhudi za kuzuia na kushughulikia unyanyasaji wa kingono na ukatili.

Bwana Atul Khare msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu msaada mashinani amesema “pamoja tumeimarisha juhudi zetu” ameuambia mkutano unaofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mastaifa ukijumuisha nchi wanachama zaidi ya 60, ikiwa ni pamoja na nchi wachangiaji wa askari wa kulinda amani na polisi.

Amesema hivi sasa kuna uwazi mkubwa katika utoaji taarifa wetu na kitengo chetu cha habari na mawasiliano , uchunguzi ama uwe wa Umoja wa Mataifa au wa nchi wanchama unakamilishwa haraka. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa hivi sasa unapanua wigo wa msaada kwa waathirika ikiwemo kupitia kuanzishwa kwa mfuko maalumu ambao amewaambi nchi waanchama unategemea msaada wao.

Pia akitambua hatua zilizopigwa mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix, ameongeza kuwa licha ya juhudi kubwa za Umoja wa Mataifa bado kuna taarifa zinazowahusisha wafanyakazi, katika vitengo vyote vya ulinzi wa amani na katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake ya karibuni Iliyotolewa 28 Februari 2017 aliainisha mikakati kwa ajili ya kuzuia na kushughulikia ukatili na unyanyasaji wa kingono .