Waafghanistan milioni 1 kupata haki ya kuishi Pakistan-UNHCR

Waafghanistan milioni 1 kupata haki ya kuishi Pakistan-UNHCR

Mipango ya Pakistan ya kuorodhesha hadi raia milioni moja wa Afghanistan wasio na nyaraka za kuishi nchini Pakistan itatoa afuweni kubwa inayohitajika kwa wakimbizi wengi ambao hawawezi kurejea nyumbani kutokana na sababu za kiusalama umesema leo Umoja wa Mataifa.

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR , limekaribisha mradi huo wa Pakistan ambao unatoa ulinzi dhidi ya watu kukamatwa kiholela, kuwekwa rumande na au kurejesha nyumbani kwa nguvu.

Zoezi hilo la uorodheshwaji lilianza Alhamisi mjini Islamabad na mji wa Kaskazini Magharibi wa Peshawar, ambako Waafghanistan wengi wasio na vibali wanaishi. Duniya Aslam Khan ni msemaji wa UNHCR

(DUNIYA KHAN CUT)

"Ni hatua muhimu sana kwa sababu Waafghan wengi nchini Pakistan wanaweza kushindwa kurejea nyumbani Afghanistan hivi karibuni ukizingatia hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya Afghanistan. Mwaka jana ulikuwa mgumu sana kwa Waafghanistan walioko Pakistan , Waafghanistan 370,000 walioorodheshwa ambao walisafirishwa na Waafghan laki sita ambao hawajaorodheshwa walirejea Afghanistan kutoka Pakistan na sababu zikiwa mabadiliko ya kikanda, uhusiano baina ya Afghanistan na Pakistan, shinikizo kutoka kwa mamlaka, kubalidi mtazamo kwa jamii zinazowahifadhi, kutokuwa na uhakika wa kusailiwa tena kadi zao za ukimbizi, ugumu wa kiuchumi na udhibiti wa mipakani.”