Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen inakabiliwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu- WHO

Yemen inakabiliwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu- WHO

Yemen inakabiliwa na mlipuko mkubwa zaidi wa kipindupindu kuwahi kushuhudiwa duniani huku kukiwa na visa 368,207 vinvyoshukiwa na vifo 1,828 vilivyoripotiwa tangu Aprili 27 mwaka 2017. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa Shirika la afya ulimwenguni WHO, kila siku waYemeni 5,000 zaidi wanaugua ugonjwa wa kuhara au kipindupindu, huku watoto walio chini ya umri wa miaka 15 wakiwa ni asilimia 41 ya visa vilivyoripotiwa. Nao watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60 wakijumuisha theluthi moja ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu.

Kwa sasa nusu ya vituo vya afya nchini Yemen vimefungwa au havitumiki kikamilifu, na hivyo kuwaacha watu takriban milioni 15 bila huduma za msingi za afya.

WHO imesema watu milioni 14.4 hawana huduma ya maji safi na kujisafi kwa sababu ya kusambaratika kwa miundombinu.