Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lacroix azuru Darfur Sudan:UNAMID

Lacroix azuru Darfur Sudan:UNAMID

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix leo amewasili El Fasher mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan kwa ajili ya ziara ya siku mbili.

Ziara yake imekuja wakati ambapo kuna mipango ya kufanya mabadiliko katika mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kulinda amani Darfur UNAMID ili ukidhi mahitaji ya sasa ya kudumisha na kulinda amani Darfur.

Muda mfupi baada ya kuwasili Bwana Lacroix alikutana na gavana wa Elfasher Abdul Wahid Yusub Ibrahim na kisha kuzungumzia walichojadili.

(LACROIX CUT)

“Tumejadili matarajio ya mabadiliko ya UNAMID na ushirikiano tutakaoendelea nao ili kwamba mipango ya amani itekelezwa kwa utaratibu na bila purukshani. Pia tumejadili mipango ya kuendelea kusaidia jamii hususan wakimbizi wa ndani , kuwajengea uwezo katika masuala ya utawala wa sheria na kuwsaidia kuboresha usalama.”