Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya watoto Zanzibar ni msingi mzuri wa kumsaidia mtoto

Mahakama ya watoto Zanzibar ni msingi mzuri wa kumsaidia mtoto

Zanzibar-Tanzania hatua kubwa imepigwa katika ulinzi wa watoto baada ya kufungua mahakama tatu mpya kwa ajili ya kuwalinda watoto na haki zao, mahakama ambazo zinatumika kusikiliza na kutoa hukumu za kesi zinazowahusu watoto chini ya umri wa miaka 18.

Bi. Nyezuma Simai Issa, Afisa Hifadhi ya Mtoto katika Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii, Zanzibar amezungumza na Amina Hassa wa idhaa hii na kuanza kumfafanulia umuhimu wa kuanzishwa mahakama hizo