Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa chakula uliosahaulika DRC wahitaji kutupiwa jicho:FAO

Mgogoro wa chakula uliosahaulika DRC wahitaji kutupiwa jicho:FAO

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kutosahau mamilioni ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao walikimbia vita na sasa wanakabiliwa na njaa.

Ombi hilo limetolewa na afisa wa tathimini ya mgogoro wa chakula wa shirika la chakula na kilimo (FAO), Luca Russo.

Amesema watu milioni sita raia wa DRC wako ukimbizini au wanaishi katika makambi kutokana na vita kwenye maeneo matatu nchini mwao ambayo ni majimbo ya Kasaï ,Tanganyika na Kivu upande wa Mashariki.

Mwana Russo Russo alikuwa DRC kama sehemu ya mpango wa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula (WFP) na FAO.

Ameongeza kuwa wakati dunia inajikita na baa la njaa linalonukia Sudan Kusini, Somalia, Yemen na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria , DRC isipewe kisogo..

(RUSSO CUT)

“Kama umetawanywa kwa sababu wa vita  na huwezi kulima upataji wako wa chakula unakuwa finyu na athari za vita hivi inachangiwa pia na mgogoro wa kiuchumi wa Congo kwa sasa, hivyo uwezo wa kununua hasa kwa makundi yasiyojiweza umetharika na hali hii. Wengi wa watu hawa wameshindwa kuvuna kwa misimu mitatu iliyopita ya upanzi, hii imeleta athari kubwa kwa chakula.”