Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira kwa vijana bado ni chagamoto nchini Burundi

Ajira kwa vijana bado ni chagamoto nchini Burundi

Moja ya changamoto kubwa inayowakumba vijana wengi duniani ni ukosefu wa ajira. Nchini Burundi, asilimia takriban 22 ya vijana waliohitimu vyuo vikuu hawajapata ajira. Kwa mujibu wa Serikali ukosefu wa kazi ni tishio kubwa kwa ustawi wa jamii nchini humo. Baadhi ya mashirika ya kiraia nchini Burundi yameanza kuwahamasisha vijana na kuwaelekeza jinsi ya kubuni ajira ili kukabiliana na ukosefu mkubwa wa kazi. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA akiwa mjini Bujumbura Burundi ametuandalia makala hii . Jiunge naye.