Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 316 warejeshwa Somalia kwa msaada wa IOM

Wahamiaji 316 warejeshwa Somalia kwa msaada wa IOM

Baada ya karibu miezi 5 ya kusubiri, wahamiaji 316 wa Kisomali wamerejea nyumbani kupitia Bahari ya Arabia wakisaidiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji , IOM katika kipindi cha siku nne zilizopita.

Mnamo Februari mwaka huu, boti ya walanguzi iliokuwa imebeba Wasomali 150 ililipitia kweye Pwani ya Yemen ikielekea Ulaya.

Kwa bahati mbaya boti hiyo ilishambuliwa kilomita chache tu kutoka Pwani, ambapo wahamiaji 40 waliuauwa na wengine 13 kujeruhiwa.

Manusura 90 walisafirishwa na IOM kutoka Al Hudaydah hadi Sana’a, mji mkuu wa Yemen.

Na Julai 14, watu hao wakiwemo watoto 8 waliwasili kwenye Pwani ya Berbera, Somalia. Kikundi kingine cha wahamiaji 103 kiliondoka Eden July 15.

Tangu Novemba 2016 jumla ya Wasomali 1,306 wamerejea nyumbani wakisaidiwa an Shirika la IOM na wadau wake.