Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tubadili mtazamo na kubaini mizizi ya migogoro Afrika:Guterres

Tubadili mtazamo na kubaini mizizi ya migogoro Afrika:Guterres

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kubadili mtazamo wake kuhusu bara ka Afrika na kuanzisha ushirika wa ngazi ya juu ambao utatambua uwezo na ahadi kubwa za bara hilo. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo kwenye mjadala maalumu wa baraza la usalama kuhusu kuimarisha uwezo wa Afrika katika masuala ya amani na usalama.

Amesema katika suala hilo Afrika na Umoja wa mataifa wanafikra za pamoja katika kuboresha njia za kuzuia migogoro kabla haijashika kasi na kuidhibiti pindi inapotokea, na hivyo...

(GUTERRES CUT 1)

"Kuimarisha uwezo wa Afrika ni muhimu katika mtazamo wa wajibu wetu wa pamoja kukabiliana na changamoto za amani na usalama wa kimataifa pamoja na kujitegemea kwa bara la Afrika."

Ameongeza kuwa miziz ya fitna inayochangia chokochoko ni muhimu sana ikakatwa

(GUTERRES CUT 2)

"Tunahitaji kubaini mizizi ya migogoro, tushirikiane kwa karibu kuwa na tathimini ya pamoja, kubadilishana taarifa na kujaribu kufikia muafaka utakaosaidia hatua za mapema ikiwemo uongozi bora na upatanishi, masuala ya uchaguzi, haki za binadamu na misaada ya kibinadamu."

Amesema masuala mengine pia yanayotishia usalama na amani ya kimataifa kama vile suala la ugaidi na itikadi kali lazima yatupiwe jicho.