Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kuendelea kuisaidia Haiti ikijiweka sawa: MINUSTAH

Ni muhimu kuendelea kuisaidia Haiti ikijiweka sawa: MINUSTAH

Msaada wa kimataifa kwa Haiti utakuwa muhimu sana wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea kukamilisha ufungaji wa mpango wake nchini humo ,amesema afisa wa ngazi ya juu wa mpango huo kwenye baraza la usalama hii leo.

Sandra Honoré mkuu wa MINUSTAH, amesema mpango huo utafunga mlango wake kabisa mwezi Oktoba mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na mpango wa operesheni za ufuatiliaji ambao utajikita zaidi katika masuala ya utawala wa sheria na haki za binadamu.

Ameongeza kuwa taifa hilo lipo katika njia muafaka ya kurejesha utulivu na demokrasia lakini ameonya kwamba kutokuwepo na hatua zinazoonekana katika nyanja ya utawala wa sheria kuna athari mbaya katika maisha ya watu na haki zao za binadamu.

(SANDRA HONEREE CUT)

‘Mchakato wa uchaguzi uliokuwa karibu kakamilika mapema mwaka huu umefungua ukurasa wa kisiasa kwa serikali mpya , kuanza kushughulikia changamoto nyingi zinazoikabili nchi hiyo, kwa kutumia fursa hii ya kipekee kushughulikia mizizi ya kutokuwepo utulivu, umasikini, watu kutengwa na ukwepaji sheria.”