Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kutengeneza mkaa kupitia taka za minazi waleta nuru Mombasa, Kenya

Mradi wa kutengeneza mkaa kupitia taka za minazi waleta nuru Mombasa, Kenya

Tuzo ya SEED inatolewa kila mwaka kwa miradi inayochagiza maendeleo endelevu na inayojali mazingira. Tuzo hiyo inatolewa kwa miradi bunifu katika nchi zinazoendelea ambayo ina uwezo wa kubadili maisha katika juhudi za kutokomeza umaskini na kuhifadhi mazingira. Mmoja wa washindi wa mwaka huu ni Shukry Said Twahir kutoka kampuni ya Kencoco ya Kenya, ambaye amehojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa hii kwanza anaanza kwa kuelezea mradi wake uliomfanya ashinde tuzo hiyo.