Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumuenzi vyema Mandela sio kwa maneno bali kwa vitendo-Guterres

Kumuenzi vyema Mandela sio kwa maneno bali kwa vitendo-Guterres

Nelson Mandela anaendelea kuchagiza dunia kupitia mifano aliyokuwa nayo ya ujasiri , utu na juhudi zake za kupigania haki za kijamii, kitamaduni na amani. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Nattss, Nelson Mandela......

Ni Nelson Mandela akizungumza alipohutubia baraza kuu Oktoba 3 , 1994 kama Rais wa kwanza kutoka Afrika Kusini kufanya hivyo .

Leo hii katika siku ya kimataifa ya kumenzi Mandela leo hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, Katibu Mkuu Antonio Guterres amesema kila wakati alipokutana na Mandela...

(GUTERRES CUT 1)

Nilipigwa na butwaa kutokana na hekima yake, huruma yake, na zaidi ya yote, unyenyekevu wake. Ameongeza kuwa moja ya funzo kubwa ambalo watu wanaweza kujifunza kutoka kwa Mandela ni kupiga hatua na ni lazima kusonga mbele licha ya changamoto zozote zitakazojitokeza.

Nelson Mandela wakati mmoja alisema “mtakatifu anaweza kuelezewa kuwa ni mwenye dhambi anayeendelea kujaribu". Huo ni ujumbe mzito wa matumaini amesema Guterres hasa katika dunia hii iliyojawa na hofu na kiburi.

Akisema bado hatujachelewa kujaribu tena na kuchukua hatua kuukabili mustakhbali wa dunia hii na kwamba leo hii tunapomuenzi Mandela..

(GUTERRES CUT 2)

“Kila mmoja wetu anaweza kuleta mabadiliko kwa kuchagiza amani , haki za binadamu, maendeleo endelevu na maisha ya utu kwa wote. Kila mmoja wetu anaweza kuhamasishwa na mifano ya Mandela na kauli yake maarufu: kila wakati inaonekana haiwezikani hadi pale itakapofanyika”

Nelson Mandela aliaga dunia nyumbani kwake nchini Afrika Kusini tarehe 5 Decemba 2013, na Umoja wa Mataifa ulitenga tarehe 18 July kilwa mwaka kuwa ni siku ya kumuenzi Mandela kwa yale aliyoyamini na kuyatenda.