Ukombozi wa Mosoul haujamaliza changamoto zote Iraq: Kubiš
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema ukombozi wa kihistoria wa Mosul usifunike ukweli kwamba mustakhbali wa taifa hilo bado unakabiliwa na changamoto nyingi. Akihutubia baraza la usalama hii leo Ján Kubiš amesema ukombozi wa Mosul ulifanikiwa kwa juhudi kubwa za majeshi ya ukombizi ya Iraq na wadau wa kimataifa ili kuwaokoa na kuwalinda watu wa taifa hilo .
Hata hivyo amesema taifa hilo litaendelea kuhitaji msaada wa kimataifa ikiwemo kuondoa mabomu ya ardhini yaliyoachwa na magaidi na kuwarejesha mamelfu ya wakazi waliozikimbia nyumba zao. Ameongeza kuwa sula la ukombozi wa maeneo mengine ambayo bado yanashikiliwa na Daesh nacho ni kibarua kigumu
(KUBIS CUT )
“Ukombozi wa maeneo mengine ambayo bado yanadhibitiwa na Daesh kama sehemu ya majimbo ya Ninewa, Ambar, Havijah jimbo la Kirkuk na majimbo mengine haitakuwa rahisi, zaidi ya hapo wafuasi wa Daesh wanaendelea na vitendo vya kikatili Iraq na kwengineko.”