Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yamepitisha viwango vya matumizi ya dawa zitumikazo kwa mifugo

Mashirika ya UM yamepitisha viwango vya matumizi ya dawa zitumikazo kwa mifugo

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia matumizi ya dawa katika bidhaa za mifugo zitumikazo kama chakula na kwa mimea wamepitisha viwango vinavyodhibiti matumizi ya dawa hizo, katika mkutano uliofanyika leo huko Geneva Uswisi.

Muafaka huo umefikiwa kufuatia utafiti wa pamoja wa kamati ya Shirika la chakula duniani FAO na lile la afya ulimwenguni WHO kuhusu tembe zinazoongezwa kwenye vyakula.

Miongoni mwa dawa zilizowekewa viwango ni dawa ijulikanayo kama Ivermectin inayotumika kuua vimelea kwenye tishu za mifugo na nyingine ni Lasalocid sodium inayoua vimelea kwa ndege ikiwemo kuku na batamzinga pia viwango vimewekwa dhidi ya matumizi ya teflubenzuron inayotumika kwa samaki aina ya chache.

Kadhalika kamisheni hiyo iliyoanza kikao chake cha 40, imepitisha viwango dhidi ya dawa zaidi ya 25 zinazotumika kuua wadudu kwa baadhi ya vyakula ikiwemo matunda na mboga mboga na bidhaa zitokanazo na mifugo ikiwemo maziwa na mayai.

Aidha viwango vimewekwa dhidi ya matumizi ya bidhaa zilizo na arsenic ambayo inayotumika katika mchele ambao ni chakula muhimu katika jamii nyingi kote ulimwenguni na hivyo matumizi yake yanahatarisha watu wengi kiafya na huathiri upatikananji wa mchele na hivyo kutishia uhakika wa chakula.