Kutimiza SDG’s lazima kasi ya utekelezaji iongezeke:Guterres

17 Julai 2017

Kama dunia inataka kutokomeza umasikini, kukabili changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuwa na jamii jumuishi zenye amani kwa wote ifikapo 2030, basi wadau wote muhimu wakiwemo serikali, ni lazima waongeze kasi ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Wito huo umo katika ripoti mpya ya tathimini ya utekelezaji wa SDG’s iliyozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Ripoti hiyo inatoa mtazamo wa utekelezaji wa malengo hayo duniani ikitaja maeneo yaliyopiga hatua na kule ambako juhudi zinahitajika zaidi kuhakikisha hakuna atakeyesalia nyuma.

Guterres amesema ripoti imebaini kwamba wakati kuna hatua zilizopigwa katika muongo mmoja katika kila nyanja ya maendeleo , kasi ya hatua hiyo haitoshelezi na haiwiani kuweza kutekeleza malengo hayo. Ameongeza kuwa saa zinasonga na hatua lazima zichukuliwe sasa

(GUTERRES CUT 1)

"Nchi zinazoendelea lazima zitekeleze wajibu wake kuhusu msaada wa maendeleo, lakini wakati huohuo hii haitoshi kufadhili malengo ya maendeleo, ni lazima tuweke mazingira yatakayozisaidia nchi kukusanya rasilimali zake zenyewe , lakini pia kuchagiza jumuiya ya kimaptaifa kupambana kwa pamoja dhidi ya ukwepaji kodi, usambazaji fedha haramu na uzuiaji haramu wa mitaji.”

Amesema la msingi tusiangalie tuu ya leo tugange pia yajayo..

(GUTERRES CUT 2)

‘Nchi, mashirika ya kimataifa yasiweze tu kuchukua hatua za sasa bali pia kuona mbali , nini kinakuja na kuwekeza katika elimu , ujuzi mpya, na mabadiliko ili soko la ajira liweze kwenda sanjari na mabadiliko yajato.”