Utalii wanufaisha wakaazi nchini Tanzania

14 Julai 2017

Utalii!. Idadi ya watalii wa kutoka nje ya bara la Afrika imeongezeka tangu mwaka 1995. Mfano kati ya 1995 hadi 1998 idadi imeongezeka kutoka Milioni 24 hadi takribani watalii milioni 56 kati ya mwaka 2011-2014. Takwimu za baraza la kimataifa la safari na utalii linasema idadi ya watalii wa kigeni barani Afrika inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni 134 mwaka 2030. Nchi zilizopata watalii wengi ni pamoja na Rwanda, Uganda na Tanzania.

Zaidi ya hilo, Sekta ya utalii ni chanzo muhimu cha ajira Afrika. Utalii umeongeza pato la ndani la bara la Afrika kutoka wastani wa dola bilioni 69 kati ya 1995–1998 hadi dola bilioni 166 kati ya mwaka 2011–2014. Inakadiriwa kuwa pato hilo litaongezeka muongo ujao na kufikia dola bilioni 269 mwaka 2026.

Utafiti wa Ripoti mpya ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kuhusu maendeleo ya uchumi Afrika umebaini kuwa wanawake wanastawi zaidi kwenye sekta ya utalii. Jane Muthumbi, Afisa uchumi wa UNCTAD kitengo cha Afrika anaanza kwa kutueleza mchango wa sekta hii katika ustawi wa wanawake nchini Tanzania