Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhil kwa raia Kasai DRC hayana dalili ya kupungua-UNHCR

Madhil kwa raia Kasai DRC hayana dalili ya kupungua-UNHCR

Madhila kwa maelfu ya watu wanaoendelea kutawanya na machafuko katika jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hayana dalili ya kupungua limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Katika eneo hilo linaloshuhudia machafuko tangu mwishoni mwa 2016, idadi ya watu waliotawanywa UNHCR inasema sasa imefikia milioni 1.3 na wengi wankimbilia majimbo mawili yaliyo mpakani na Kasai ya Kwilu na Lualaba.

Kwa mujibu wa UNHCR watu waliokutana nao katika majimbo hayo wengi wao walisafiri kwa wiki kadhaa msituni bila chakula, maji ya kunywa, dawa wala mavazi, huku wenzao wakifariki dunia njiani wakiwemo wanawake na watoto.

Pia majeraha ya waathirika wengi ni ya kukatwa mapanga au kupigwa risasi, William Spindler ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA SPINDLER)

“Hatari ya unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji inaifanya hali hiyo kuogofya zaidi. Watoto na wanawake wengi walikimbia peke yao. Watoto wengine wasiokuwa na wazazi au walezi hawana mipangilio yoyote ya huduma kwa watoto na wengi wa wale waliokimbia makazi yao wanahifadhiwa na jamii zilizowapokea licha kuwa zina rasilimali ndogo."