Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Silaha za nyuklia ni mwiba unaopaswa kutolewa

Silaha za nyuklia ni mwiba unaopaswa kutolewa

Silaha za nyuklia zimekuwa mwiba kwa wakazi wa dunia hii hasa kwa wale ambao silaha hizo zimetumika na kuwaletea madhara, mathalani huko Hiroshima na Nagasaki nchini Japan. Madhara kama vile watoto kuzaliwa na ulemavu wa viungo, wanawake kushindwa kubeba ujauzito ni miongoni mwa madhara lukuki yaliyosababisha Umoja wa Mataifa kupitia nchi wanachama wake kukutana kwenye makao makuu jijini New York, Marekani kwa takribani wiki tatu kuanzia katikati ya mwezi Juni mwaka huu na hatimaye kupitisha mkataba wa kutokomeza silaha hizo. Ingawa baadhi ya nchi kama vile Marekani na Israel hazikushiriki mjadala huo, bado washiriki wamesema ni mafanikio makubwa.

Je ni kipi kimefanikiwa? Linnet Ng'ayu kutoka baraza la viongozi wa dini barani Afrika ACRL-RfP nchini Kenya ameshiriki mkutano huo na anamweleza Assumpta Massoi wa Idhaa hii kile walichojadili, mambo yaliyozua utata na hata mwelekeo wa baadaye. Lakini anaanza kwa kueleza kilichowagusa zaidi.