Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kifo cha mwanaharaki wa Uchina ni pigo kwa haki za binadamu duniani-Zeid

Kifo cha mwanaharaki wa Uchina ni pigo kwa haki za binadamu duniani-Zeid

Mwanaharakati wa Uchina wa amani na demokrasia aliyeaga dunia , Liu Xiaobo ameenziwa na kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akisema alikuwa ni “Ufafanuzi wa ujasiri wa kiraia na heshima ya kibinadamu."

Bwana Liu, aliyekuwa na umri wa miaka 61, amekuwa akisumbuliwa na saratani ya ini na ameaga dunia leo Alhamisi mjini Shenyang, Kaskazini Mashariki mwa Uchina.

Alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 11 jela na alipewa msamaha kwa ajili ya matibabu mwezi Juni mwaka jana baada ya ugonjwa huo kufikia hatua mbaya.

Bwana Liu alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2010 akiwa jela. Kamishina mkuu wa haki za binadamu , Zeid Ra'ad Al Hussein ametoa taarifa akiomboleza kifo chake , na kukiita kuwa ni pengo kubwa katika vuguguvu la haki za binadamu China na duniani kote.

Ameongeza kuwa "Liu Xiaobo alikuwa mshairi na mwanazuoni aliyetaka na kupigania mustakhbali bora kwa nchi yake.

Zeid amesema Liu ataendelea kuwa hamasisho na mfano wa kuigwa kwa wote wanaopigania haki za binadamu.