Miradi ya Kenya, Uganda ni miononi mwa washindi 15 wa tuzo ya SWITCH-UNEP
Mradi wa mifuko itokanayo na shina la mgomba wa ndizi nchini Kenya, mradi wa madawati ya shule yaliyotengenezwa kwa taka za plastiki kutoka Burkina Faso, mradi wa kuboresha maisha ya wakulima wa kahawa na usalama wa sokwe wa mlimani Uganda ni miongoni mwa washindi 15 wa tuzo ya kifahari ya mwaka huu ijulikanayo kama SWITCH Africa Green SEED.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP, washindi hao wametangazwa katika kongamano la ngazi ya juu la kisiasa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.
Tuzo za SEED ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa kutambua miradai inayoanza ya ubunifu ambayo inajali mazingira katika nchi zinazoendelea na tuzo hizo zinasaidia kukuza miradi hiyo na kuifanya kuwa mfano wa kuigwa. Rainer Agster afisa wa SEED..
(AGSTER CUT)
"Tunalenga mada kuanzia ubunifu na uiigaji, jinsi gani unaweza kuiga mifano ya biashara zilizofanikiwa kutoka eneo moja, kanda moja au nchi moja"
Miradi hiyo 15 iliyoshinda ilichaguliwa na na jopo huru la majaji wataalamu wa kimataifa , kutoka zaidi ya washindani 300. Miradi yao inajumuisha kilimo, udhibiti wa taka, nishati, uzalishaji, bayoanuai na utalii.