Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uthubutu wa kutekeleza yanayosemwa utafanikisha SDGs- Moshi

Uthubutu wa kutekeleza yanayosemwa utafanikisha SDGs- Moshi

SDGs.(Picha:UNIC/Tanzania)Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs uko katika mstari sahihi nchini Tanzania kufuatia sera mpya zilizopo za kuhakikisha ulinzi wa mapato ya kitaifa.

Hiyo ni kauli ya Celestine Moshi, mkurugenzi, idara ya ushrikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, akizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs unaondelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Bwana Moshi amesema Tanzania imeweka mikakati ili kuhukikisha kwamba malengo hayo yanafikiwa

(Sauti ya Moshi)

Aidha amezungumzia matarajio yake kutoka kwenye mkutano

(Sauti ya Moshi)