Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Cyprus wamalizika bila muafaka

Mkutano wa Cyprus wamalizika bila muafaka

Mazungumzo yaliyolenga kuweka mwelekeo wa kuwezesha Cyprus kuungana tena baada ya kuvunjika mapande mwaka 1974 yamemalizika bila maafikiano yoyote. Taarifa kamili na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye aliombwa kurejea Crans Montana Uswisi jana ili kushiriki mazungumzo hayo amewaambia waandishi wa habari hii leo mjini humo kuwa..

(Sauti ya Guterres)

“Nina masikitiko makubwa kuwataarifa kuwa licha ya azma thabiti na ushiriki wa pande zote, mkutano kuhusu Cyprus umefungwa ila maafikiano yoyote.”

Pande husika kwenye mazungumzo hayo ni wajumbe wa upande wa wacyprus wenye asili ya Uturuki na wale wenye asili ya Ugiriki huku waratibu wakiwa ni Ugiriki, Uturuki, Uingereza ilhali Umoja wa Ulaya ni mwangalizi.

Bwana Guterres alipoulizwa iwapo pande husika zitaendelea na mashauriano au la, amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Mkutano umefungwa. Hii haimaanishi kuwa mbinu nyingine haziwezi kuibuliwa ili kushughulikia tatizo la Cyprus. Umoja wa Mataifa ni mwezeshaji na tuko tayari kwa pande zitakazokuwa tayari kufikia makubaliano iwapo hali itakuwa hivyo.”

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari kuna baadhi ya masuala muhimu yanayozua tashwishi kubwa ni mustakabali wa askari 35,000 walioko katika kisiwa hicho.