6 Julai 2017
Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yanalenga ikiwemo: kutokomeza umaskini uliokithiri, kumaliza utofauti wa usawa wa kijinsi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Usawa wa kijinsia ni miongoni mwa masuala muhimu kwa ajili ya kufikia ajenda ya 2030. Huku upatikanaji wa ajira ukiwa ni changamoto hususan katika nchi zinazoendelea mazingira duni ya kazi pia ni tatizo. Hilo limeibuka katika simulizi hii ya Flora Nducha ikiangazia wanawake ambao wamepoteza ajira hivi karibuni nchini Kenya kama moja ya juhudi za kupaza sauti za wanawake na shirika linalohusika na maswala ya wanawake UN-Women kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma.