Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sauli aeleza ndoto zake za kubadlisha maisha ya vijana na jamii Tanzania

Sauli aeleza ndoto zake za kubadlisha maisha ya vijana na jamii Tanzania

Umoja wa Mataifa hivi sasa unapigia chepuo ushirikishaji wa vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Malengo hayo ni mtambuka ambapo vijana wanaweza kushiriki katika kufanikisha malengo yote iwapo watajiongeza. Mathalani huko Tanzania kijana mmoja amejiongeza na kupigia chepuo lengo namba nne la linalotaka elimu jumuishi na yenye usawa. Kijana huyo Saul Mwame wa kidato cha nne katika shule ya sekondari DCM Mvumi, Dodoma hajasubiri usaidizi bali amejipa changamoto na kuanza kusonga mbele kama anavyotanabaisha katika mahojiano yake na Joseph Msami. Anaanza kwa kueleza anavyojihisi kupata fursa ya kuhutubia Umoja wa Mataifa.