Mkurugenzi Mkuu mpya wa WHO Dk Tedros aanza majukumu rasmi

2 Julai 2017

Hii leo Julai mosi, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus amenza kazi rasmi akiwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, akichukua nafasi ya Dk Margaret Chan ambaye ameshikilia wahdifa huo kwa miaka kumi.

Dk Tedros mzaliwa wa Ethiopia, atakayeshikilia wadhifa huo kwa miaka mitano, alichaguliwa na nchi wanachama katika uchaguzi wa baraza kuu la WHO mnamo Mei 23 mwaka huu. Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza kwa shirika hilo kujumuisha wagombea wengi, kwani awali utaratibu ulikuwa bodi ya WHO kutuma jina kwa baraza la shirika hilo ili kulipitisha.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO ni mkuu wa masuala ya kifundi na utawala, pia husimamia sera za shirika katika kazi zake za afya kimataifa.

Ddk Tedros amewahi kushika nyadhifa kadhaa mchini Ethiopia ikiwamo Waziri wa mambo ya nje kuanzia mwaka 2010 hadi 2016 ambapo moja ya jukumu alilolitekeleza ni kuongoza majadiliano ya ajenda yaa Addis Ababa, yaliyofikiwa kwa nchi 193 kuahidi uwezeshaji wa kifedha kwa ajili ya kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu SDGs.

Mkuu huyo mpya wa shirika la afya ulimwenguni WHO, alikuwa waziri wa afya wa Ethiopia mwaka 2005 hadi 2012. Alifanya kazi kubwa ya kuongoza juhudi za kuunda upya mfumo wa afya wa Ethiopia ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu ya afya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter