Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ndogo ndogo na mchango wake katika fursa za ajira

Biashara ndogo ndogo na mchango wake katika fursa za ajira

Juni 27 ni siku ya kimataifa ya biashara ndogo ndogo na zile za wastani. Siku hii ambayo imeadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu wa 2017 baada ya kupitishwa na azimio la Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa inalenga kuhimiza umuhimu wa sekta ya biashara ndogo ndogo na zile za wastani katika kutimiza maendeleo endelevu.

Biashara hizi hutoa fursa za ajira kwa takriban watu 250 na ni uti wa mgongo wa uchumi katika mataifa mengi kote ulimwenguni huku zikitoa mchango muhimu katika nchi zinazoendelea.

Biashara hizi zinatajwa kuwa muhimu katika ajira na fursa za kujipatia kipato na ni muarobanini katika kukabiliana na umaskini na kuchagiza maendeleo, hasa lengo namba Nane la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, biashara ndogo ndogo na za wastani, rasmi na zisizo rasmi zinajumuisha asilimia 90 ya biashara zote na kwa wastani huajiri asilimia kati ya 60-70 ya jamii huku zikichangia asilimia 50 katika pato la ndani la taifa, GDP.

Tayari mashirika ya Umoja wa Mataifa yamezindua mkakati wa kimataifa wa kuhakikisha kazi bora kwa vijana ili kuinua ajira kwa kundi hilo ambalo sasa linakabiliwa na changamoto Je hali ya ajira kwa vijana ikoje hususan Afrika Mashariki? Tunaanzia nchini Tanzania ambako Dotto Bulendu wa radio washirika Radio SAUT ya Mwanza ameandaa ripoti ifuatayo……………….

[Radio SAUT PKG]

Nako nchini  Kenya, Vincent Monda ambaye ni mwandisi wa habari mafunzoni chini ya uratibu wa Geoffrey Onditi kutoka radio washirika Shirika la utangazaji nchini Kenya, KBC amezungumza na baadhi ya vijana ambao wanajihusisha na biashara ndogo ndogo.

[PACKAGE VINCENT]