Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mzozo, wakimbizi wa Syria warejea nyumbani- UNHCR

Licha ya mzozo, wakimbizi wa Syria warejea nyumbani- UNHCR

Idadi ya raia wa Syria wanaoishi ukimbizini nje ya nchi yao au wale walio wakimbizi wa ndani imeripotiwa kuimarika.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema wakimbizi hao wanarejea kwa hiari kwa mipango yao wenyewe ambapo sababu kubwa ni kuangalia makazi yao au familia zao huko Aleppo, Hama, Homs na Damascus baada ya mapigano yanayokumba nchi yao.

Mashirika ya misaada yanakadiria kuwa kwa mwaka huu pekee zaidi ya wakimbizi wakimbizi wa ndani 440,000 wamerejea makwao huku wengine 31,000 wakiwa ni wale waliotoka nje ya nchi.

Kufuatia kurejea huko, UNHCR imeimarisha operesheni zake za usaidizi ndani ya Syria ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao ikiwemo huduma za malazi na ulinzi.