Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenyeji na wakimbizi wagombania rasilimali Bunj, Sudan Kusini-UNHCR

Wenyeji na wakimbizi wagombania rasilimali Bunj, Sudan Kusini-UNHCR

Wakati mzozo wa Sudan Kusini ukizidi kushika kasi, katika mji mdogo uitwao Bunj,uliopo jimboni Uppern Nile, nuru inaangaza kwani msimu wa mvua umeleta ahueni kutokana na maporomoko ya maji yanaleta uzima kwa nyasi na mazao ambazo awali zilikauka.

Lakini licha ya hayo,uwepo wa wakimbizi zaidi ya 140,000 waliojihifadhi humo kuanzia mwaka 2013 pale mapigano yalipoanza, unadidimiza ustawi wa wenyeji ambao nao wanasaka maisha bora.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, uwepo wa wakimbizi umeongeza kero kutokana na kuibuka mapigano ya kikabila katika kambi zao pamoja na mapigano dhidi ya jamii wenyeji.

Andreas Fiadrome ni Afisa Mkuu wa ulinzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

(Sauti Andreas)

‘‘Bunj ni mji mdogo wenye rasilimali chache sana kama vile maji, huduma za afya, elimu, huduma ambazo haziitoshi jamii ya hapo. Na sasa uwepo wa wakimbizi unachochea mgogoro kati yao na jamii wenyeji. Wenyeji wanawatizama wakimbizi kama wavamizi au wanaowania rasilimali hizo chache.’’

UNHCR kwa kushirikiana na mamlaka ya eneo hilo, imelazimika kuunda baraza la pamoja la amani, ili kusaidia makundi yote kufanya kazi pamoja hadi pale wakimbizi watakaporejea makwao salama, kwa utu na tumaini la mustakabali mwema.