Wakimbizi wa Nigeria wasilazimishwe kurejea makwao- UNHCR

29 Juni 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeonya juu ya hatua yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi wa Nigeria walioko nchini Cameroon kurejea makwao.

Katika taarifa yake ya leo, UNHCR imesema wakimbizi hao wanalazimishwa kurejea kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambako mazingira hayajawekwa sawa ili kuwapokea.

Onyo hili la sasa limetolewa wakati tayari takribani wakimbizi 900 wa Nigeria wengi wao wakiwa ni watoto wakiwa wamerejeshwa nchini mwao kwa lazima Jumanne wiki hii.

UNCHR imesema hali ya kutokuwepo kwa usalama kwenye ukanda huo inakwamisha nia ya wakimbizi kurejea makwao na hivyo wasilazimishwe kwa kuwa watajikuta wanaishia kwenye mji wa mpakani wa Banki.

UNHCR imesema mji wa Banki tayari unahifadhi wakimbizi zaidi ya 45,000 na wanaishi kwenye mazingira ya mlundikano wakiwa hawana maji safi na salama.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter