Bila kuhusisha elimu ya mtoto wa kike SDG’s haziwezi kufikiwa: UNESCO

29 Juni 2017

Elimu ya mtoto wa kike ni muhimu sana katika kusaidia kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG, ifikapo mwaka 2030. Hayo yamesemwa na mkuruguenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova kwenye mkutano maalumu unaofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, hii leo kuhusu lengo la maendeleo nambari 4 linalohusu elimu

(BOKOVA CLIP)

“Bila kuhusisha wasichana katika elimu, bila kushungulikia vikwazo muhimu katika elimu yao kama ubaguzi, vikwazo vya umasikini, ukabila, dini, hatuwezi kufikia uendelevu katika malengo yoyote ya elimu na malengo mengine ya maeendeleo endelevu.”

Naye naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohamed anayehusika hasa na ufuatiliaji wa utimizaji wa malengo hayo katika elimu anasema

(AMINA CLIP)

“Tumekosa wasichana wengi sana na elimu lazima iwe kwa wotete wawili, na kama tunataka kutoa fursa kwa vijana kukua na kuongoza nchi zao, elimu ni ufunguo katika hilo.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter