Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukanda wa tropiki kujadili changamoto na fursa

Ukanda wa tropiki kujadili changamoto na fursa

Kwa mara ya kwanza kabisa, Siku ya kimataifa ya nchi zilizo kwenye ukanda wa tropiki inaadhimishwa leo, hizi ni nchi zilizo kati ya tropiki ya cancer na ile ya Capricorn.

Maeneo ya Tropiki ni yale ambayo licha ya mabadilko ya hali ya hewa hushuhudia joto na mara chache hali ya hewa hubadilika kwa misimu, na kilicho cha upekee kwa maeneo hayo ni uhifadhi wa mvua katika maeneo yenye unyevu karibu na Ikweta na kuongezeka kwa mvua za msimu kulingana na umbali kutoka Ikweta.

Siku ya kimataifa ya Tropiki inasherehekea utofauti wa ajabu wa kitropiki ilihali ikianisha changamoto na fursa ambazo mataifa yaliyo kwenye ukanda huo hukabiliana nazo.

Katika siku hii, ukanda wa tropiki hutoa fursa za kupiga hatua kwa kushirikishana habari na utaalamu na kutambua utofauti na umuhimu wa ukanda huo