Kasi yahitajika ili nchi 44 ziridhie CTBT

29 Juni 2017

Mkutano wa wataalamu wenye lengo la kubadilishana ujuzi juu ya ufuatiliaji majaribio ya nyuklia ukiendelea huko Vienna, Austria, mshiriki kutoka Kenya ametoa wito kwa ushirikiano zaidi ili nchi nyingi zaidi ziridhie mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya silaha hizo, CTBT.

Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kando ya mkutano huo, mshiriki kutoka Kenya, Magdalene Wangui ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi amesema viongozi na wananchi wapigie chepuo..

(Sauti ya Magdalene)

Hadi sasa nchi 180 zimetia saini mkataba huo wa CTBT na nyingine tayari zimeridhia. Hata hivyo ili uanze kutumika ni lazima nchi 44 ziridhie na miongoni mwao ni China, Marekani, Misri, Iran na Israel.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter