Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumieni fursa hii muhimu kwa ajili ya amani Cyprus-Guterres

Tumieni fursa hii muhimu kwa ajili ya amani Cyprus-Guterres

Pande zote katika mazungumzo ya Cyprus lazima zitumie fursa hii ya kihistoria kufikia muafaka, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Jumatano.

Ujumbe wake umewasilishwa Uswis na Jeffrey Feltman, msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa , katika mazungumzo yaliyoanza tena mjini in Crans-Montana kuhusu mgawanyiko wa kisiwa cha Cyprus.

Bwana Feltman amewaambia waandishi wa habari kwamba masuala kadhaa yanahitaji kufanyiwa maamuzi ikiwemo suala la kushirikiana madaraka, mipaka, na mali. lakini sasa ni wakati wa viongozi wa pande mbili husika kuamua kuhusu mtazamo wa pamoja wa hatma ya taifa lao.

Jeffrey Feltman ameongeza kuwa António Guterres anataka pande zote husika kutumia fursa hii ya kipekee kutatua tatizo ambalo limedumu kwa zaidi ya nusu karne.

Hata hivyo amesema kuta matumaini

(SAUTI YA FELTMAN)

“Tulichokisikia asubuhi ya leo kimetupa matumaini na uhakika kwamba viongozi na wadhamini watatu wamekuja kwenye mkutano huu na nia ya kukabili changamoto na kutatua matatizo.”

Wanaoshiriki mkutano huo unaoongozwa na Umoja wa Mataifa ni pamoja na wahusika wakuu kiongozi wa Cyprus ya Ugiriki Nicos Anastasiades, mwenzie wa Cyprus ya Uturuki Mustafa Akinci, Muungano wa Ulaya, na wadhamini watatu ambao ni Ugiriki, Uturuki na Uingereza.