Mkutano wa ustawi wa wahamiaji waanza Ujerumani

28 Juni 2017

Mkutano wa siku tatu kuhusu maendeleo ya wahamiaji hususani mitizamo chanya kwa kundi hilo umeanza mjini Berlin nchini Ujerumani, ambapo kiwa ni siku ya kwanza wito wa kuhakikisha wahamiaji wananufaika na jamii wanakoishi umetolewa.

Viongozi katika ufunguzi wa mkutano huo wametoa ahadi za kuimarisha usimamizi kwa wakimbizi kimataifa, na ustawi wa kiuchumi kwa wahamiaji.

Mkutano huo uko chini ya uenyekiti wa Morocco na Ujerumani ambapo, mwakilishi wa serikali ya Morocco El Habib Nadir, amesema ni kwa juhudi za pamoja pekee na kuhuisha ushirikiano kwaweza kunufaisha wahamiaji katika nchi wanakohifahdiwa na zile walikotoka.

Viongozi wanaotarajiwa kuhutubia ni pamoja na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Louise Arbour na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji William Lacy Swing

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter