Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa kijinsia wakumbwa na vikwazo- Wataalamu

Usawa wa kijinsia wakumbwa na vikwazo- Wataalamu

Harakati za kusongesha haki za wanawake zinakabiliwa na vikwazo vikubwa maeneo mengi duniani, wamesema wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo.

Katika taarifa yao iliyotolewa Geneva, Uswisi, wataalamu hao wa kikosi kazi cha udhibiti wa ubaguzi dhidi ya wanawake kisheria na kivitendo, wamesema dunai sasa iko njiapanda kwa kuwa hoja ya usawa wa kijinsia inakabiliwa na vikwazo kila uchao.

Wamesema kuna mvutano mkubwa ambapo baadhi ya makundi yanatumia visingizio vya dini na utamaduni kusigina haki za wanawake huku serikali nyingine nazo zikitumia mabavu yao.

Hata hivyo wamepongeza baadhi ya nchi ambazo zimefuta sheria ambazo zinakwamisha usawa wa kijinsia na hata kuharamisha vitendo au tabia za wanawake na wasichana.

Wataalamu hao ni Karima Bennoune, Ahmed Shaheed, Vitit Muntarbhorn na Dubravka Šimonoviæ.