Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bima ya afya ndio muarobaini wa afya kwa wote- Tanzania

Bima ya afya ndio muarobaini wa afya kwa wote- Tanzania

Jukwaa la afya barani Afrika likikunja jamvi hii leo huko Kigali nchini Rwanda, Tanzania imesema moja ya suluhu za kudumu ya afya kwa wote ni kuwa na bima ya afya kwa kila mwananchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya  amesema hayo akihojiwa na Idhaa kutoka Kigali, Rwanda ambako anahudhuria jukwaa la kwanza la Afrika kuhusu afya, suala la afya kwa wote likipatiwa kipaumbele.

(Sauti ya Dkt. Mpoki)

Kuhusu mbinu za teknolojia za Uganda za kubaini selimundu na Kifuakikuu pamoja na ile ya Kenya ya MTiba Dokta Mpoki amesema..

(Sauti ya Dkt. Mpoki)