Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres ziarani Washington DC

Guterres ziarani Washington DC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani kwenye mji mkuu wa Marekani, Washington DC akisaka kufahamisha wajumbe wa baraza la Kongresi la nchi hiyo kuhusu umuhimu wa kazi za umoja huo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephané Dujarric amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa hii leo Bwana Guterres amekutana na zaidi ya wajumbe 20 wa kamati ya mambo ya nje ya baraza hilo la Kongresi..

(Sauti ya Dujarric)

“Katibu Mkuu amejadili juhudi za marekebisho ya Umoja wa Mataifa, ajenda yake ya kinga na ushirikiano chanya wa Marekani na Umoja wa Mataifa na vitisho vitokanavyo na ugaidi duniani.”

Amesema Katibu Mkuu ameshukuru wajumbe wa baraza hilo kwa ukarimu na usaidizi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa na amebadilishana nao mawazo kuhusu masuala mbali mbali yenye umuhimu duniani.