Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tathimini ya hatua ya kupinga majaribio ya nyuklia yafanyika Vienna

Tathimini ya hatua ya kupinga majaribio ya nyuklia yafanyika Vienna

Wataalamu kutoka kila pembe ya dunia wanakutana mjini Vienna, Austria, wiki hii ili kubadilishana ujuzi na maendeleo ya teknolojia katika kufuatilia majaribio ya nyuklia.

Mkutano huo wa sayansi na teknolojia 2017 ni miongoni mwa msururu wa mikutano yenye lengo la kuimarisha utekelezaji wa mkataba unaopinga majaribio ya nyuklia (CTBT) ambao unapiga marufuku milipuko ya nyuklia popote pale duniani.

Zaidi ya mataifa 180 yametia saini mkataba wa Umoja wa Mataifa , wengi wao wameshauridhia mkataba huo. Hata hivyo mkataba huo bado unahitaji kuridhiwa na nchi zingine 44 kabla haujaanza kutekelezwa .

Hiki ni kikao cha sita cha mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ambao kwa mara ya kwanza pia kimejumuisha mtazamo maalumu kuhusu vijana na wanasayansi vijana.