Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kuheshimu na kuthamini mchango wa mabaharia-IMO

Ni muhimu kuheshimu na kuthamini mchango wa mabaharia-IMO

Likitanabaisha changamoto zinazowakabili mabaharia, wanawake kwa wanaume wanaosafiri na kufanyakazi ndani ya meli , shirika la kimtaifa la wanamaji IMO, liometoa wito wa kuthamnini mchango wa watu hao.

Katika kuadhimisha siku ya mabaharia duniani ambayo kila mwaka huwa Juni 25, Katibu Mkuu wa IMO, Kitack Lim amesema “ingawa ubaharia unaweza kuwa msingi wa kutosheleza ajira ya muda mrefu, bado ni vigumu na ni kazi inayohitaji muda mwingi.

Katika ujumbe wake wa siku hii ameongeza kuwa mbali ya masuala binafsi, hali ndani ya meli na bandarini ,kutolipwa mishahara na hata kutelekezwa, mabaharia wanakabiliana na hali ya kuwa mbali na familia na marafiki zao na shinikizo la kufanya kazi katika mazingira magumu ya kiuchumi ambayo yanawaongezea adha.

Bwana . Lim amesisitiza kuwa ni rahisi kwa baharia kuhisi mpweke na aliyetengwa akifikiria kwamba hana thamani. Hivyo amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni kuonyesha kwamba “mabaharia ni muhimu”.