Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo na majeruhi kwenye ajali ya gari la mafuta Pakistan vimenistua:Guterres

Vifo na majeruhi kwenye ajali ya gari la mafuta Pakistan vimenistua:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi kufuatia kulipuka kwa lori la mafuta karibu na mji wa Ahmedpur Mashariki wilaya ya Bahawalpur jimbo la Punjab nchini Pakistan.

Kupitia taarifa ya msemaji wake Katibu Mkuu ametuma salam za rambirambi kwa watu na serikali ya Pakistan kufuatia kisanga hicho na amewatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada kwa serikali ya Pakistan endapo utahitajika.

Zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha katika ajali hiyo na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.