Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twaunga mkono mpango wa Katibu Mkuu kwa Haiti- Baraza

Twaunga mkono mpango wa Katibu Mkuu kwa Haiti- Baraza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza azma yake ya kufanikisha utekelezaji wa mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja huo katika kukabiliana na ugonjwa kipindupindu nchini Haiti.

Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Juni Balozi Sacha Llorenti amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Port au Prince nchini Haiti, mwishoni mwa ziara yao ya siku tatu nchini humo.

Balozi Llorenti amesema hatua hiyo inafuatia kile walichoshuhudia na kusikia kutoka kwa wananchi ikiwemo waathirika wa kipindupindu ambapo suala kubwa ni fidia ikiwemo miradi ya kujikwamua kiuchumi.

Kuhusu mwelekeo wa Haiti wakati huu ambapo ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSTAH unatarajiwa kuhitimisha shughuli zake na ujumbe mwingine mdogo zaidi MINUJUSTH kuanza majukumu yake Oktoba 15 mwaka huu, Balozi Llorenti amesema wameelezwa kuwa mchakato uko vizuri na kwamba…

(Sauti ya Balozi Llorenti)

Haiti kwa bahati nzuri imeingia zama mpya ya utulivu na hivyo kutoa fursa nzuri kwa serikali na taasisi nyingine kuweza kuleta mipango ya marekebisho inayohitajika ili Haiti iweze kuingia katika mwelekeo wa maendeleo endelevu.”