Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya kidijitali yanasua wakazi wa Afrika Mashariki

Biashara ya kidijitali yanasua wakazi wa Afrika Mashariki

Hivi karibuni kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezindua ripoti yake kuhusu mwelekeo wa uwekezaji duniani kwa mwaka huu wa 2017.

Kubwa lililomulikwa katika ripoti hiyo ni namna biashara ya kidijitali  inavyokuwa kwa kasi. mathalani watu hununua vitu mitandaoni na kufikishiwa majumbani kwao.

UNCTAD imetaka wafanyabiashara hususani nchi zinazoendelea kutumia fursa hiyo kunufaika na biashara hiyo.

Afrika Mashariki biashara hii imeanza kushamiri ambapo kwa kutumia teknolojia na mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, Whatsapp na mingineyo wafanyabishara husaka wateja kwa kuweka bidhaa zao sokoni huku pia malipo yakifanyika kutumia simu za mikononi.