Kitendo cha kutesa hakiwezi kuhalalishwa kamwe

Kitendo cha kutesa hakiwezi kuhalalishwa kamwe

Katika kuadhimisha Siku ya Kupinga Mateso hii leo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema hata kama mataifa yataendelea kutumia mateso kwa kisingizio cha ulinzi wa taifa, bado msimamo ni ule ule, wa kuwa mateso ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mataifa hayo ni lazima yatokomeze hali hiyo.

Wamesema sheria za uzuiaji wa mateso ni halisi, na haviwezi kamwe kusadikishwa katika hali yoyote, huku wakizikumbusha nchi kuwa hakuna hali ya kipekee ambayo inaweza kuingizwa ili kuhalalisha vitendo vya utesaji, hata iwe ni katika mazingira ya kupambana na ugaidi, na kwamba uvumilivu wa tabia za kuadhibu kiholela zikiendelea basi mataifa yataelekea katika mteremko wa kurejesha na kuhalalisha utesaji.

Kwa mantiki hiyo wamesema nchi zinapaswa kuimarisha uzuiaji kabisa wa vitendo hivyo, kukumbuka majukumu yao katika kutenda na kutumia mikataba ya kimataifa na itifaki zilizopo, na wajibu wao wa kuchunguza na kutoa ufanisi wa haraka katika suala hili ikiwa ni pamoja na kuwafidia waathirika wa mateso na familia zao.