Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchafuzi wa udongo ni hatari kwa mimea-FAO

Uchafuzi wa udongo ni hatari kwa mimea-FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya kuwa uchafuzi wa udongo utokanao na shughuli za kibinadamu una madhara ya moja kwa moja kwa chakula na afya ya binadamu.

FAO imesema hayo wakati wa mkutano wa tano wa kimataiaf kuhusu ubia wa udongo uliofanyika mjini Roma Italia, ikitolea mfano wa kemikali kama vile zebaki na nyinginezo zaweza kuathiri mfumo wa uzalishaji wa mimea na kusababisha madhara kwenye ardhi na kuathiri vyanzo vya maji, na hata ustawi wa vijijini unaotegemea kilimo.

Shirika hilo limeshauri kwamba njia pekee ya kukabiliana na changamoto hiyo inayoongezeka kwa kasi ili kukuza udongo endelevu ni kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kujenga ushahidi wa kisayansi juu ya madhara hayo.

Kukabiliana na uchafuzi wa udongo na kuhakikisha uendelevu katika udongo ni muhimu katika kutimiza maendeleo endelevu SDGs amenukuliwa Rattan Lal, Rais wa shirika la kimataifa la muungano wa sayanasi ya udongo.