Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo la kimataifa kuchunguza ukatili Kasai, Zeid apongeza

Jopo la kimataifa kuchunguza ukatili Kasai, Zeid apongeza

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio hii leo kuunda jopo la kuchunguza madai ya ukatili kwenye majimbo yaliyoko eneo la Kasai huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein amekaribisha hatua hiyo akisema itatoa fursa ya kuepusha ukwepaji sheria na ni matumaini yake DRC itapatia jopo hilo fursa ya kufika maeneo yote.

Tangu mwaka jana watu milioni 1.3 ni wakimbizi wa ndani huko Kasai na wengine 30,000 wamekimbilia Angola.

Akizungumzia hatua hiyo, Mwakilishi wa DRC kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi Zénon Mukongo Ngay amesema..

(Sauti ya Zénon)

“Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na inakubali kupokea jopo hilo la wachunguzi la Umoja wa Mataifa linalokuja kusaidia suala la haki DRC kwa kuangazia ukatili uliotokea Kasai.”