Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilio cha wajane hakisikiki na hakijaliwi

Kilio cha wajane hakisikiki na hakijaliwi

Leo ni siku ya wajane duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ingawa jukumu la wajane ni kubwa na muhimu katika jamii, bado umuhimu wao hauonekani kwani wamesahaulika, hawamo katika utafiti wala takwimu zozote na haki zao zinapuuzwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Nats..

Ni kilio cha Margaret, mjane mwenye watoto saba ambaye alinyanga'nywa mali na watoto wake wa kiume baada ya mumewe kufariki dunia, mali ambazo anasema yeye na mumewe walifanya kazi kwa pamoja kuzipata.

Umoja wa Mataifa unasema vitendo kama anavyofanyiwa Margaret pamoja na vingine kama vile kunyimwa urithi wa ardhi, kunyimwa haki ya kuomboleza na kushiriki mazishi, kufukuzwa nyumbani na hata kuonekana na nuksi hadi pale mjane anapokubali kuolewa na ndugu wa mumewe ni ukatili unaokabili kundi hili.

Akihojiwa na idhaa hii Margaret anasema anahangaika pekee kwani..

(Sauti ya Margaret-1)

Na ni ujumbe gani anatoa kwa wajane wenzake..

(Sauti ya Margaret-2)