Ziara ya Guterres Imvepi yawapa matumaini wakimbizi

22 Juni 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres leo amezuru kambi ya wakimbizi ya Imvepi iliyoko Arua Kaskazini mwa Uganda. Kambi hiyo inahifadhi maelfu ya wakimbizi Kutoka Sudan Kusini.

Amepata fursa ya kusikiliza kilio chao n ahata kuwagawia mgao wa chakula. Flora Nducha amezungumza na mwandishi wetu John Kibego aliyeko Imvepi kufuatilia ziara hiyo na anaeleza hali ilivyokuwa

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa nchini Uganda alipotembelea kambi ya Imvepi iliyoko wilaya ya Arua.(Picha:UM/Mark Garten)

(MAHOJIANO NA KIBEGO)Mara baada ya kuzungumza na wakimbizi hao wa Sudan Kusini, Katibu Mkuu alizungumza na waandishi wa habari akisema..

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa nchini Uganda alipotembelea kambi ya Imvepi iliyoko wilaya ya Arua.(Picha:UM/Mark Garten)

(Sauti ya Guterres)“Kile tulichoshuhudia sote ni ukarimu wa kipekee wa wananchi wa Uganda na serikali yao kuwapokea kama ndugu zao mamia ya maelfu ya wakimbizi, karibu milioni moja kutoka Sudan Kusini na kutumia pamoja ardhi na kila kitu walichonacho katika dunia ambayo watu wengi wabinafsi wanafungia milango wakimbizi. Huu ni mfano wa pongezi na kuigwa na jamii ya kimataifa.”

Katibu Mkuu ambaye miaka 12 iliyopita akiwa Kamishna Mkuu wa wakimbizi alitembelea eneo hilo na kukutana na wakimbizi wa Sudan Kusini na hata wakati wa shamrashamra za kuelekea uhuru wao mwaka 2011 amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Kwa bahati mbaya viongozi wa Sudan Kusini hawajawapatia wananchi wao kile wanachotaka. Wamepata machungu na vita hivi visivyokwisha. Ni wakati wa viongozi wote wa Sudan Kusini kumaliza vita hivi.”

Naye Waziri Mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda pamoja na kushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuwezesha nchi hiyo kusaidia wakimbizi, amesema wanashirikiana na jirani zake pamoja na mamlaka ya IGAD na Muungano wa Afrika ili kusaka suluhu ya mzozo wa Sudan Kusini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter