Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri isitishe hima kunyonga watu sita-UM

Misri isitishe hima kunyonga watu sita-UM

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Misri kusitisha hukumu ya kunyongwa kwa watu sita nchini humo baada ya mwenendo wa kesi zao kutokidhi viwango vya kimataifa vya haki.

Jopo hilo katka taarifa yake limeeleza masikitiko yake likisema watu hao wanaume, wamehukumiwa kwa misingi ya kulazimishwa kukiri.

Kuendelea kwa adhabu hiyo ya kuyongwa kwa watu hao kwa misingi ya kesi mbaya, kutavunja haki za binadamu za kimataifa, na kuchangia mauaji ya kiholela, wamoenya wataalamu hao ambao wamejikita katika mauaji,utesaji,uwekwaji kizuizini na kukabiliana na ugaidi.

Adhabu ya kifo kwa kundi hilo ilitolewa na mahakama kuu ya Misri mnamo Juni saba mwaka huu, ambapo watuhumiwa hao walishitakiwa mwaka 2015 wakihusishwa na ugaidi hasa wakihusishwa na mauaji ya afisa wa polisi mwaka 2014.