Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha G-5 ruksa kupambana na ugaidi Sahel:

Kikosi cha G-5 ruksa kupambana na ugaidi Sahel:

[caption id="attachment_303576" align="aligncenter" width="625"]overnightmali

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja Jumatano jioni limepitisha azimio la kuanzishwa kikosi cha pamoja cha nchi za Sahel zijulikanazo kama G-5. Mapema Februari mwaka huu nchi za G-5 ambazo ni Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger ziliamua kuunda kikosi cha pamoja ili kukabiliana na tishio la ugaidi na April Muungano wa Afrika uliidhinisha uamuzi huo.

Katika azimio hilo nambari 2359 baraza la usalama linakaribisha kupelekwa kikosi cha takribani watu 5000 wakiwemo wanajeshi na polisi katika ukanda huo. Na limetoa wito kwa nchi kutoa msaada wa kiufundi na fedha kusaidia kikosi hicho.

Pia azimio hilo linataka kudumishwa ushirikiano baina ya kikosi hicho kipya na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA na pia kikosi cha Ufaransa Barkhane. Francoise Delattre ni balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa mataifa

(SAUTI YA FRANCOISE)

Azimio lililopitishwa (2359) linatoa msaada wenye nguvu katika hatua kubwa ya Afrika" na linachangia mbinu ya kimkakati katika kuhamasisha nia ya nchi za Afrika kuchukua jukumu la usalama wa bara lao."