Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda kuendesha mkutano wa mshikamano na wakimbizi, ambao idadi yao inaongezeka

Uganda kuendesha mkutano wa mshikamano na wakimbizi, ambao idadi yao inaongezeka

Uganda inakuwa mwenyeji wa mkutano wa siku mbili wa mshikamano na wakimbizi , kwa msaada wa Umoja wa Mataifa katika wakati ambao mgogoro wa wakimbizi nchini humo unashika kasi.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, wimbi kubwa la wakimbizi wa Sudan Kusini limeongeza karibu mara mbili idadi ya wakimbizi wanaohifadhiwa nchini Uganda na kufikia zaidi ya milioni 1.2.

Mkutano utakaofanyika Juni 22 na 23 utawaleta pamoja wakuu wa nchi 30 na wahisani wa kimataifa, ambao wanatarajiwa kuchangisha dola bilioni 2 ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya wakimbizi na jamii zinazowahitaji.

UNHCR inasema idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaoingia Uganda inatarajiwa kuongeza.